Wasifu wa Demba Ba

Imebadilishwa: 22 Novemba, 2012 - Saa 09:38 GMT
Demba Ba

Demba Ba

Demba Ba ameonyesha uwezo, dhamira na nia ya kucheza vyema ili kujihakikishia nafasi katika kikosi cha Newcastle, baada ya kukumbana na wakati mgumu.

Huenda ni kutokana na uwezo huo alioonyesha ambao umevutia macho ya wengi na kumwezesha kuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa timu hiyo msimu huu.

Mshambuliaji huyo kutoka Senegal mwenye umri wa miaka 27, alionyesha uwezo mkubwa katika timu ya Newcastle alipojiunga nayo kutoka West Ham mwezi Juni 2011.

Amefunga magoli 16 msimu wake wa kwanza akiwa mfungaji anayeongoza japo alipata wakati mgumu aliporejea kutoka mashindano ya 2012 ya mataifa bingwa barani Afrika na kuiwezesha Newcastle kumaliza ya tano katika ligi kuu ya England na kupata fursa ya kucheza kombe la Uropa.

Licha ya kutokuwa miongoni mwa wachezaji wa kwanza kumi na mmoja wa Newcastle mara kwa mara katika mechi za ligi kuu ya premier msimu huu,Demba Ba amefunga magoli nane katika mechi 12 alizocheza na kumwezesha kuwa mfungaji bora wa timu ya Newcastle na mfungaji wa pili bora katika ligi kuu.

Ba, ambaye alizaliwa Ufaransa, alianza kuchezea timu ya taifa ya Senegal, maarufu kama Simba wa Teranga, katika mchezo wake na Tanzania mwezi Juni 2007, na amefunga magoli manne katika timu hiyo baada ya mechi zake 16.

Amekuwa sehemu ya washambuliaji maarufu wa timu ya Senegal, akipigania nafasi ya ufungaji na mchezaji mwenzake wa timu ya New Castle Papiss Cisse, Moussa Sow na Dame N'Doye na Moussa Konate.

Lakini Ba na wachezaji wenzake mwaka ujao hatawataonekana na timu yao ya Senegal katika mashindano ya mataifa bingwa Afrika, yatakayofanyika nchini Afrika Kusini, baada ya Senegal kushindwa kufuzu kwa sababu ya vurugui zilizojitokeza katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Ivory Coast.

Badala yake, Ba ataelekeza macho yake katika timu yake ya Newcastle katika kinyang'anyiro cha msimu huu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.