Wasifu wa Didier Drogba

Imebadilishwa: 22 Novemba, 2012 - Saa 09:15 GMT
Didier Drogba

Didier Drogba

Mwezi Mei mwaka huu, Didier Drogba, alikihama klabu ya Chelsea baada ya kuichezea kwa muda wa miaka minane.

Drogba alitajwa kuwa mchezaji bora zaidi wakati wa mechi ya fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya ambapo Chelsea, iliibuka na ushindi.

Baada ya kupewa kadi nyekundi katika fainali ya mashindano hayo miaka minne iliyopita, Drogba alifunga penalti ya mwisho na kuipa Chelsea ushindi wake wa kwanza katika fainali hizo.

Baada ya kandarasi yake na Chelsea kumalizika, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, aliamua kujiunga na klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki katika mechi ya ligi kuu nchini Uchina.

Ripoti zinasema kuwa Drogba alijiunga na klabu hiyo baada ya kusaini mkataba wa pauni elfu mia mbili kwa wiki na tayari ameifungia klabu hiyo magoli 11.

Umaarufu aliouonyesha Drogba, wakati wa fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya mjini Munich, Ujerumani, ulikuwa kinyume kabisa na wakati alipokuwa akiichezea timu ya taifa ya Ivory Coast, wakati wa michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

Drogba naodha wa Ivory Coast

Drogba aliongoza kikosi hicho cha Ivory Coast kufikia fainali ya mashindano hayo kwa mara ya pili.

Didier Drogba

Didier Drogba

Na kama ilivyokuwa katika fainali ya mashindano hayo nchini Misri, miaka sita iliyopita, fainali hiyo iliamuliwa kwa njia ya penalti.

Kwa katika mechi hiyo, Zambia ambayo haikutarajiwa na wengi kushinda, ilivunja ndoto ya Drogba ya kushinda kombe hilo na timu yake ya taifa.

Wakati alipokuwa akiichezea Chelsea, Drogba alifunga zaidi ya magoli 150 na kucheza takriban mechi 350.

Alishinda kombe la ligi kuu ya premier mara tatu, kombe la Fa mara nne na kombe la ligi mara mbili.

Mwezi Oktoba mwaka huu mashambiki wa Chelsea walipiga kura ambapo aliibuka kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo.

Drogba alishinda taji la BBC la mchezaji bora barani afrika mwaka wa 2009 na licha ya kukumbwa na masaibu katika maisha yake, Drogba hakupoteza muda na nafasi aliyopata na kujikakamua na kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi kutoka Afrika.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.