Sifa za Yahya Toure

Imebadilishwa: 22 Novemba, 2012 - Saa 09:47 GMT
Yahya Toure

Yahya Toure

Baada ya kuisaidia klabu yake ya Manchester City, kushinda kombe lake la kwanza kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka thelathini na tano, Yahya Toure, aliibuka kua mmoja wa wachezaji nyota wa klabu hiyo katika michuano ya kuwania kombe la ligi kuu ya premier msimu uliopita, ambapo pia Manchester City waliibuka washindi wa ligi hiyo kwa mara ya kwanza.

Mcheza kiungo huyo kutoka Ivory Coast, alikuwa nyota wa Manchester City katika harakati zake za kumaliza ukame wa kutoshinda kombe la ligi kwa zaidi ya miaka ya 44.

Ushupavu wa mchezaji huyo, pamoja na mfumo wake wa kuwakabili vikali wapinzani wake na nguvu aliyo nayo uliisaidia Manchester City kuthibiti safu ya kati kabla ya kuwapiki wapinzani wao.

Na wakati michuano ya ligi ilipopamba moto, Toure aliibuka mchezaji bora wakati timu yake ilipoilaza mahasimu na majirani wao wa Jadi Manchester United na pia alifunga mabo mawili wakati wa mechi yao ya pili kabla ya ligi kumalizika dhidi ya Newcastle, matokeo yaliyoiweka Manchester City Kileleni mwa msururu wa ligi kuu ya Premier, kwa wingi wa mabao, hali iliyowafanya kutwaa kombe hilo.

Ushindi huo unaongezeka, idadi ya medali aliyoshinda mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Medali nyingine alizoshinda ni pamoja na kombe la klabu bingwa barani ulaya, kombe la bara ulaya la Super Cup, kombe la klabu bingwa duniani, mawili ya ligi kuu ya premier ya Uhispania na lile la Copa DeL Rey aliloshinda akiwa na Barcelona, bila kusahau kombe la ligi kuu ya premier ya Ugiriki akiwa na klabu ya Olimpiakos.

Toure pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2011 na shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF, na ameanza msimu huu kwa vishindo.

Alifunga bado wakati wa mechi ya kuwania kombe la Charity Sheild au Ngao ya Jamii, wakati Manchester City ilipoibuka na ushindi dhidi ya Chelsea.

Kufikia sasa Toure amefunga jumla ya magoli manne kwenye ligi kuu ya premier.

Mwezi Januari Toure anatarajiwa kuakilisha Ivory Coast kwenye michuana ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.