Maelezi kumhusu Younes Belhanda

Imebadilishwa: 22 Novemba, 2012 - Saa 10:01 GMT
Younes Belhanda

Younes Belhanda

Wakati mchezaji mkongwe Zinedine Zidane alikisifu talanta yako, basi jua kuwa unafanya jambo nzuri kama mchezaji wa soka, na Younes Belhanda kwa hakika amekuwa na msimu ambao ataishi akiukumbuka.

Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 22, alikuwa mmoja wa wachezaji waliotia fora na kuisaidia klabu ya Montepellier, kushinda kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya karne moja tangu klabu hiyo ilipobuniwa.

Akicheza safu ya kati, nyuma ya mshambulizi Olivier Giroud, mchezaji huyu kutoka Morocco, alifunga jumla ya magoli 12 kutokana na mechi 26, saba yakiwa ndio mabao yalitofufua matumaini yao ya kutwa kombe hilo, mara tu aliporejea, kutoka kuiwakilisha taifa lake katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

Mchezaji huyo mwenye kipaji na talanta ya soka, alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotia fora katika kikosi cha Morocco kilichoshiriki katika michuano ya kuwania komba la Mataifa bingwa barani Afrika mwaka wa 2012.
Alifunga bao la ushindi wakati wa mechi yao dhidi ya Nigeria na pia kutoa pasi iliyosababisha bao wakati wa mechi yao na Gabon.

Lakini ni kutokana na juhudi zake katika klabu ya Montpellier, iliyoshinda kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza ndizo zilizompa umaarufu mkubwa na kuteuliwa katika kikosi cha wachezaji 11 bora wanaoshiriki katika ligi ya Ufaransa pamoja na tuzo la mchezaji bora chipukizi.

Heshima kama hiyo imewahi kutunukiwa wachezaji kama vile Eden Hazard, Franck Ribery, Thierry Henry na Zidane na hivyo Belhanda sasa ni miongoni mwa wachezaji walioko katika orodha hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.