Chelsea itaimarika-Benitez

Imebadilishwa: 26 Novemba, 2012 - Saa 13:59 GMT
Kocha wa Chelsea

Kocha wa Chelsea

Kocha mpya wa Chelsea, Rafael Benitez amesisitiza kuwa atafanikiwa kuzima uhasama kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo, ambao walimpokea huku wakiwa wamebeba mabango ya kumsifu kocha laiyefutwa kazi.

Mashabiki hao walimzomea Benitez, wakati alipojitokeza katika eneo linalotumiwa na maafisa wa kiufundi, na mashabiki wengine walimtusi wakati wa mechi yao dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City hiyo jana ambapo timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya kutofungana bao lolote.

'' wakati mashabiki wanapoimba kuniunga mkono au kunikashifu, mimi sijali chochote. Kile ninachokitaka ni kubadili maoni yao'' alisema Benitez.

Aliongeza kusema kuwa atafanya hivyo kwa kujitahidi zaidi na kuhakikisha kuwa Chelsea imeshinda mechi zake.

Kocha wa Chelsea

Tazama Benitez Kocha mpya wa Chelsea akizungumza baada ya mechi yao na Manchester City katika uwanja wao wa Stampford Bridge.

Mashabiki wa Chelsea

Benitez ana uhakika kuwa atabadili mawazo ya mashabiki hao wa Chelsea, ambao waliimba kushinikiza kurejesha kwa Kocha aliyefutwa kazi, Roberto Di Matteo, ambaye alifutwa na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich miezi sita ti baada ya kushinda kombe la FA na pia lile la klabu bingwa barani Ulaya.

Banitez alisema ''nitazingatia sana mbinu za kuimarisha mchezo wetu na sitatumia muda wangu kuzingatia masuala mengine ambayo hayataimarisha matokeo yetu''

''Nimekuwa hapa England kwa miaka minane na nimesikia mambo mengi. Wataona kuwa mimi ni mtu ninayezingatia maadili ya utendaji kazi na nitafanya kazi yangu kwa nguvu zangu zote na kadri ya uwezo wangu wote''

Kocha huyo aliongeza kuwa baada ya kuona mechi yao dhidi ya Manchester City, ana uhakika kuwa Chelsea, itaanza kushinda mechi zake zijazo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.