Dua kwa Chelsea Denmark

Imebadilishwa: 5 Disemba, 2012 - Saa 13:37 GMT

Timu ya Chelsea ina kibarua kigumu usiku wa leo

Kufuatia marufuku yake, David Luiz yuko huru kushiriki mechi ya mwisho ya Chelsea katika ligi ya Klabu Bingwa barani ulaya, dhidi ya FC Nordsjaelland, uwanjani Stamford Bridge.

Luiz alikosa mechi ya ligi ya Uingereza Jumamosi dhidi ya West Ham, baada ya kupata kadi tano za manjano.

John Terry (goti) Frank Lampard (paja) na Daniel Sturridge (mguu) wako karibu kupona lakini mechi hiyo dhidi ya mabingwa wa Denmark inawadia mapema sana.

Chelsea inahitaji kuishinda Nordsjaelland na kuomba kuwa Shakhtar Donetsk itaishinda Juventus.

Matokeo mengine yoyote yatamaanisha Chelsea itakuwa bingwa mtetezi wa kwanza wa kombe hilo kushindwa kufuzu kwa raundi ya 16 bora, kwenye msimu ufuatao

Kaimu mkufunzi wa Chelsea Rafael Benitez amekiri kuwa The Blues inahitaji " bahati kidogo" lakini akaongeza " sidhani kwamba itakuwa miujiza"

"Lazima tutekeleze kazi yetu na kusubiri (matokeo) ya timu hizo nyingine." Benitez, ambaye hajashinda mechi yoyote tangu kuanza kuifunza Chelsea, alisema haogopi kwamba Shakhtar na Juventus zitacheza kupata sare, licha ya kuwa matokeo hayo yatafaidi timu hizo mbili.

Kikosi kinachotarajiwa: Cech, Ivanovic, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Cole, Bertrand, Mikel, Romeu, Ramires, Mata, Oscar, Hazard, Moses, Marin, Piazon, Torres, Turnbull.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.