Kilimanjaro Stars kuvaana na Zambia

Imebadilishwa: 11 Disemba, 2012 - Saa 13:15 GMT
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania

Siku chache tu, baada kumaliza katika nafasi ya nne kwenye mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup, Nchini Uganda, Timu taifa ya Tanzania iantarajiwa kurejea kambini kwa maandalizi ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika Zambia.

Kwa mujibu wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Tanzania, Kilimanjaro Stars itavaana na Chipolopolo tarehe 22 mwezi huu katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha mkuu, Kim Poulsen tyari ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachopiga kambi kujiandaa kwa mechi hiyo.

Aidha kwa mara ya kwanza kikosi hicho kinajumishwa wachezaji waliotia for a kwenye michuanp ya ligi kuu na pia michuana ya CECAFA.

Miongoni mwa wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni pamoja na Aishi Manul, Samih Nuhu, Issa Rashid na Mcha Khamis.

Sita kati yao ni miongoni mwa wachezaji walioakilisha Zanzibar katika michuano ya CECAFA iliyomalizika siku ya Jumamosi jijini Kampala, Uganda, ambapo Zanzibar ilimaliza katika nafasi ya tatu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.