Wachezaji kufunzwa maadili ya Uingereza

Imebadilishwa: 11 Disemba, 2012 - Saa 12:43 GMT
Luis Suarez na Patrice Evra

Luis Suarez na Patrice Evra

Vyama vinavyosimamia mchezo wa soka katika mataifa mbali mbali, vinachunguza uwezekano wa kuanzisha mafunzo ya kijamii kwa wachezaji wa kigeni, kama njia moja ya kukabiliana na kuongezeka kwa visa vya ubaguzi wa rangi hasa nchini Uingereza.

BBC imegundua kuwa pendekezo hilo ni sehemu ya ripoti iliyotayarishwa na shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza, itakayowasilishwa kwa Waziri Mkuu David Cameron, ambaye ameitaka shirikisho la FA kuchukua hatua kali dhidi ya wale watakaopatikana na hatia.

Ripoti hiyo yenye mapendekezo 93, inajulikana kama 'English Football's Inclusion and Anti Discrimination Action Plan',pia inajumuisha mapendekezo ya vilabu vyote kuweka kipengee maalum katika kandarasi ya wachezaji na makocha wote, inayopiga marufuku ubaguzi wa rangi.

Vilabu pia vina sheria zao

Luis Suarez na Patrice Evra

Luis Suarez alikataa kjumsalamia Patrice Evra kabla ya mechi kuanza

Licha ya kuwa vilabu kadhaa huongeza sera zao, kuhusu jinsi ya kushughulikia masuala ya nidhamu ya waajiri wao, endapo kutatokea tukio lolote la ubaguzi, suala hilo sio la lazima na halijajumishwa katika kandarasi za wachezaji na makocha.

Lakini kuna pendekezo kuwa wachezaji wote wa kigeni watakaosajiliwa kucheza nchini Uingereza, wafundishwe maadili na kanuni zitakazowasaidia kuishi vyema.

Pendekezo hilo limetokea, kufuatia sakata ya ubaguzi wa rangi iliyomuhusishwa mchezaji wa Liverpool, Luis Suarez, ambaye alipigwa marufuku ya kutoshiriki mechi nane na shirikisho la FA, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya mchezaji wa Manchester United Patrice Evra.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.