Demba Ba kuhama Newcastle

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 14:40 GMT
Demba Ba

Mchezaji wa Newcastle Demba Ba

Alan Pardew yuko tayari kumsajili mshambulizi wa Ukraine Artem Milevskiy ikiwa nyota wake Demba Ba hatasaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Kocha huyo wa Newcastle ameshindwa kumshawishi Demba Ba kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Klabu hiyo sasa inashauku nyingi kuhusiana na kipengee katika mkataba wake unaosema klabu yoyote inayotaka kumsajili mchezaji huyo kabla ya muda wake kumalizika ni sharti ili pauni milioni saba ikiwa atakihama klabu hiyo mwezi Januari mwakani.

Pardew anafahamu wazi kuwa haitagharimu klabu yake hela nyingin kumsajili Milevskiy, 27, kutoka kwa klabu ya Dynamo Kiev.

Klabu hiyo iliitisha pauni milioni 14 wakati Roy Hodgson alipojaribu kumsajili mchezaji huyo akiwa na klabu ya liverpool.

Bofya Soma habari zaidi

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.