Sudan yawasilisha rufaa kwa CAS

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 17:30 GMT
Wachezaji wa timu ya taifa ya Sudan

Wachezaji wa timu ya taifa ya Sudan wakifanya mazoezi

Shirikisho la mchezo wa soka nchini Sudan, limewasilisha rufaa kwa mahakama ya upatanishi ya michezo-Cas, kupinga uamuzi wa shirikisho la mchezo huo duniani FIFA, wa kuipokonya ushindi wake katika kinyang'anyiro cha kufuzu kwa kombe la dunia, kufuatia tuhuma kuwa ilimjumuisha mchezaji ambaye hakustahili kuwepo katika kikosi chake.

Mahakama hiyo hii leo imetangaza kuwa inatarajia kutoa uamuzi wake kufikia mwisho wa mwezi Februari mwaka ujao, kabla ya michuano ya kufuzu kwa fainali hizo kuanza tena.

Sudan ilishinda Zambia kwa magoli 3-1 mjini Khartoum, tarehe mbili mwezi Juni mwaka huu, lakini FIFA, iliamua kuipa Zambia, ushindi wa mabao 3-0, baada ya kuamua kuwa Saif Ali, ambaye alifunga bao la pili, hangelishirikishwa kwenye mechi hiyo baada ya kupewa kadi kadhaa za njano katika mechi zilizotangulia.

Ali, alipewa kadi nyekundu wakati Zambia ilipoishinda Sudan katika mechi ya kufuzu kwa kombe la Mataifa bingwa barani Afrika, mwezi Februari.

Ikiwa Sudan itakabithiwa ushinda wake, itarejea tena kileleni mwa kundi lao mbele ya Ghana.

Lakini ikiwa mahakama hiyo ya Cas, itadumisha uamuzi wa FIFA, wa kuipa Zambia ushindi, Zambia itakuwa imejizolea alama sita baada ya kucheza mechi mbili.

Sudan imepangiwa kuchuana na Ghana tarehe 22 mwezi Machi mwaka ujao nayo Zambia kupepetana na Lesotho siku hiyo hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.