Amir Khan amzidi Carlos Molina

Imebadilishwa: 16 Disemba, 2012 - Saa 15:29 GMT
Amir Khan

Amir Khan akitangazwa mshindi

Katika ndondi baada ya kushindwa mapigano mawili mfululizo, Amir Khan wa Uingereza amemshinda Carlos Molina, katika pambano lililoandaliwa mjini Los angeles.

Khan, mwenye umri wa miaka 26, alipoteza mataji yake ya WBA na IBF katika uzani wa light-welterweight baada ya kushindwa na Danny Garcia na Lamont Peterson.

Lakini katika pigano hilo lililofanyika jana usiku, Khan alimuadhibu Molina kiasi cha kumlazimisha muamuzi wa pambano hilo kuisimamishwa katika raundi ya kumi ili kumuokoa Molina.

Ushindi huo ndio wa kwanza kwa Khan, ambaye kwa sasa anapewa mafunzo na Virgil Hunter na huenda akaamua kupambana na Garcia au Peterson, kujaribu kurejesha mataji yake, aliyoyapoteza.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.