Kocha wa Simba afutwa kazi

Imebadilishwa: 16 Disemba, 2012 - Saa 16:24 GMT
Aliyekuwa kocha wa Simba

Aliyekuwa kocha wa Simba

Wachezaji wa Simba wamepinga vikali uamuzi wa kamati kuu ya klabu wa kumfuta kazi kocha wa timu hiyo, Mserbia Milovan Cirkovic.

wachezaji hao wanasema Cirkovic alikuwa na uwezo na ujuzi mkubwa na pia alikuwa na ushirikiano mwema na wachezaji.

'' Kwa hakika sisi kama wachezaji tumeshangazwa sana na uamuzi wa viongozi wetu kwa kumsimamisha kazi kocha wetu ambaye tulikuwa na uhusiano mwema naye.

Lakini kwa kuwa ni uamuzi ambao sisi hatuna mamlaka juu yake itabidi kuliheshimu ila kwa manung'uniko'' alisema mmoja wa wachezaji hao ambaye hakutaka kutajwa jina.

Wachezaji wa Simba

Wachezaji wa Simba

Wachezaji qa Simba wamehoji uamuzi huo wakisema ni nadra sana kuona kocha akifutwa kazi ili hali klabu inaandikisha matokeo mena.

Lakini afisa mmoja wa klabu hiyo amesema kocha huyo amefutwa kazi kwa kuwa Simba kwa sasa haina uwezo wa kuendelea kumlipa mashahara wa kocha.

Aliongeza kuwa Kocha Cirkovic alifutwa kazi kutokana na mtindo wake wa kutozingatia mawaidha ya wasimamizi kuhusu mfumo wanaotumia hasa katika mechi za ugenini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.