Sheria dhidi ya ubaguzi kutekelezwa-FA

Imebadilishwa: 20 Disemba, 2012 - Saa 17:55 GMT
Patrice Evra na Luis Suarez

Luis Suarez akimzomea Patrice Evra

Vilabu vya Uingereza vitaadhibiwa vikiwa vitapatikana na hatia ya kutochukua hatua za kukabiliana na ubaguzi wa rangi miongoni mwa wachezaji, makocha na mashabiki, chini ya sheria mpya ya shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza.

Katika mpango ambao unatarajiwa kuwasilishwa kwa serikali, shirikisho la FA pia linatarajia kuwa na angalau asilimia kumi ya maafisa wakuu wa kiufundi na marefa kutoka kwa watu wanaotoka kabila ndogo.

Wachezaji na makocha kutoka mataifa ya nje watapewa mafunzo ya lazima kuhusu itakadi na utamaduni wa Uingereza.

Mpango huo umeafikiwa na vilabu vyote vya Uingereza, kufuatia mkutano ulioitishwa na ofisi ya Waziri Mkuu mwezi Februari mwaka huu baada ya Luis Suarez na John Terry kutuhumiwa kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya wachezaji weusi.

Mpango huo umeidhinisha na FA, Ligi kuu ya Premier, Ligi Daraja ya kwanza, chama cha wachezaji wa kulipwa PFA na chama cha makocha wa ligi kuu LMA.

Mwenyekiti wa FA, David Bernstein amesema, huo ni dhihirisho ya kujitolea kwao, kwa niaba ya mchezo huo nchini Uingereza ili kuhakikisha kuwa hakuna visa vyovyote vya ubaguzi.

Ameongeza kusema kuwa juhudi hizo zitafanikiwa ikiwa wadau wote watashirikiana kuleta mabadiliko.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.