Sturridge kusajiliwa na Liverpool

Imebadilishwa: 23 Disemba, 2012 - Saa 15:13 GMT
Daniel Sturridge

Mshambulizi wa Chelsea Daniel Sturridge

Mshambulizi wa Chelsea, Daniel Sturridge, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Liverpool hii leo kabla ya kujiunga na klabu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 12.

Liverpool, imekubaliana na chelsea kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo ya uingereza ambaye anaripotiwa kulipwa pauni elfu sitini kwa wiki.

Hata hivyo uhamisho huo hautadhibitishwa hadi mwezi ujao wakati wa uhamisho.

Mshambulizi huyo wa zamani wa manchester United amecheza mechi saba na Chelsea msimu huu.

Sturridge aliichezea chelsea mara ya mwisho wakati waliposhindwa kwa magoli 2-1 na west bromwich tarehe 17 mwezi novemba.

Sturridge hajacheza tangu rafael benitez alipoteuliwa kuwa kocha wa chelsea.

Kocha wa Liverpool, Brendan Roggers amekuwa mmoja wa makocha ambao wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo kwa muda na alijaribu kumsajili kwa mkopo mwezi Agosti lakini mchezaji huyo wa chelsea alikataa akisema anataka uhamisho wa kudumu.

Rodgers, anajaribu kuimarisha kikosi chake hasa baada ya kumruhusu Andy Caroll kujiunga na West Ham kwa mkpo mwezi Agosti.

Kocha huyo pia alishindwa kumsajili mshambulizi wa Fulham Clint Dempsey.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.