Chelsea yazidi kujiimarisha ligi kuu

Imebadilishwa: 26 Disemba, 2012 - Saa 18:00 GMT
Wachezaji wa Chelsea

Wachezaji wa Chelsea wakifurahia goli lao

Juan Mata aliifungia Chelsea bao lake la pekee na la ushindi dhidi ya Norwich, na kuiweka alama nne pekee nyuma ya mabingwa watetezi Manchester City, iliyoko katika nafasi ya pili kwa sasa.

Mata alivurumisha kombora kali kutoka umbali kwa mita ishirini na tano ambalo lilimuacha kipa wa Norwich Mark Bunn kinywa wazi.

Hata hivyo vijana hao wa Norwich, walicheza mchezo mzuri na kumfanyisha kazi ya ziada kipa wa chelsea Petr Cech.

Sebastien Bassong nusura asawazishe kwa kichwa lakini mpira ukapaa sentimita chache juu ya goli.

Katika mechi nyingine Everton imeimarisha rekodi yake ya kutoshindwa hadi mechi saba mfululizo pale ilipoifunga Wigan kwa magoli mawili kwa moja.

Everton sasa imepanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 33 baada ya kucheza mechi kumi na tisa.

Leon Osman na Phil Jagielka ndio walioifungia Everton magoli yake naye Arouna Kone aliipa Wigan bao lake la kufutia machozi.

Katika mechi nyingine Fulham imetoka sare ya 1-1 na Southampton, huku QPR ikilazwa 2-1 na West Brom, Reading ikatoka sare ya kutofungana na Swansea sawa na Aston vila na Tottenham.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.