Arsenal kutomsajili Demba Ba

Imebadilishwa: 28 Disemba, 2012 - Saa 13:47 GMT
Kocha wa Arsenal

Kocha wa Arsenal Arsene Venger

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema, hana nia ya kumsajili mshambulizi wa Newcastle Demba Ba.

Ba, 27, ameonyesha mchezo mzuri msimu huu na tayari amefunga magoli 11 msimu huu.

Mshambulizi huyo kutoka Senegal alifunga magoli kumi na sita msimu uliopita.

Kocha wa Newcastle Alan Pardew amekiri kuwa Ba, huenda akauzwa ikiwa hataondoa kipengee kimoja katika mkataba wake unaosema klabu yeyote inaweza kumsajili mchezaji huyo mradi ilipe pauni milioni saba.

''nampenda sana Demba Ba'' alisema Wenger.'' lakini ukiniuliza ikiwa tutamsajili Demba Ba basi jibu langu ni ni la''

Wenger aliongeza kusema kuwa huu sio wakati muafaka wa kuzungumzia suala hilo, kwa kuwa yeye ni mpinzani wetu kwa sasa.

Arsenal ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimehusishwa na mchezaji huyo ambaye alijiunga na Newcastle kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka klabu ya West Ham, Juni mwaka uliopita.

Wakati huo huo, Wenger amesema hajakata tamaa ya kumsajili mshambulizi wake wa zamani kutoka Ufaransa Thierry Henry, kwa mara ya tatu kwa mkataba wa muda mfupi.

Thiery ambaye aliifungia Arsenal Magoli mawili msimu uliopita, amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu kumalizika kwa ligi kuu ya Marekani MLS.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.