Kocha wa Blackbrun afutwa kazi

Imebadilishwa: 27 Disemba, 2012 - Saa 15:15 GMT
Henning Berg

Aliyekuwa kocha wa Blackburn Henning Berg

Blackburn Rovers imemfuta kazi kocha wake Henning Berg baada ya kuhudumu kwa muda wa siku 57 pekee.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43,alichukua mahala pa Steve Kean, tarehe 31 mwezi wa Kumi mwaka huu, lakini Klabu hiyo imeshinda mechi moja tu kati ya mechi kumi tangu alipoteuliwa.

Mechi ya mwisho ya Berg na klabu hiyo ilikuwa dhidi ya Middlesbrough siku ya Jumatano ambapo walilazwa bao moja kwa bila.

Wasimamizi wa klabu hiyo wanashauriana na makocha kadhaa na wanatarajiwa kumtangaza kocha mpya kabla ya mwisho wa wiki hii.

Naibu kocha mkuu Eric Black na maafisa wengine wa kiufundi Iain Brunskill na Bobby Mimms pia wamekiahama klabu hiyo ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya 17 katika ligi daraja ya kwanza.

Berg, ambaye aliongoza klabu ya aliichgezea klabu hiyo miakam ya zamani alikuwa amesaini mkataba wa miaka mitatu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.