Pardew asema Ba kusaini mkataba mpya

Imebadilishwa: 27 Disemba, 2012 - Saa 18:05 GMT
Allan Pardew

Kocha wa Newcastle Allan Pardew

Kocha wa Newcastle United Alan Pardew anataka kukubaliana mkataba mpya na Demba Ba na kukomesha uvumi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji.

Mkataba wa Demba Ba Unaruhusu mchezaji huyo kuuzwa kwa puani milioni sabab na amekuwa akihusishwa na vilabu mbali mbali ya Uingereza.

Lakini Pardew amesema ni nia yake kuafikia mkataba mpya na mchezaji huyo.

''Sisi tunatarajia kukubaliana mkataba mpya na Demba kabla ya msimu kumalizika" alisema Pardew.

Ba amefunga magoli 27 katika mechi 53 ya Ligi Kuu tangu alipojiunga na Newcastle kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka klabu ya West Ham United Juni 2011.

Vilabu vya Queens Park Rangers na Arsenal vimeonyesha nia ya kumasajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.