Man United yaendeleza ushindi wao

Imebadilishwa: 29 Disemba, 2012 - Saa 18:31 GMT
Robin Van Persie

Robin Van Persie akisherehekea bao lake

Manchester United leo imeilaza West Brom magoli 2-0 na kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier ya England, mwanzo wa mwaka ujao wa 2013.

Gareth McAuley alijifunga mwenye na kuipa Manchester United, bao lao la kwanza kabla ya Robin Van Persie kufunga bao la pili.

Baada ya mechi ishirini Mancheter United, inaongoza msururu wa ligi na alama 49, alama saba mbele ya mabingwa watetezi Manchester City.

Mabingwa hao watetezi pia walishinda mechi yao dhidi ya Norwich City kwa magoli 4-3.

Edin Dzeko alifunga magoli matatu wakati wa mechi hiyo ambayo Manchester City ilimaliza ikiwa na wachezaji kumi pekee baada ya Samir Nasri kupewa kadi nyekundu.

Matokeo zaidi

Katika mechi nyingine Cameron Jerome aliifungia Stoke City bao lake la tatu na kuinyima Southampton ushindi muhimu.

Wachezaji wa Manchester City

Wachezaji wa Manchester City

Kufuatia sare hiyo Stoke sasa imeendeleza rekodi yao ya kutoshindwa katika mechi kumi za ligi.

Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikitoshana nguvu ya kufungana magoli 3-3.

Tottenham nao waliandikisha ushindi wao wa sita kati ya mechi nane za ligi wakati walipotoka nyuma ya kufungwa bao moja na kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Sunderland.

Kufuatia ushindi huo Tottenham sasa imepanda hadi nafasi ya tatu kwenye msururu wa ligi na alama 36 alama moja mbele ya Chelsea ambayo imecheza mechi kumi na nane pekee.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.