Chelsea yailaza Everton 2-1

Imebadilishwa: 30 Disemba, 2012 - Saa 18:50 GMT
Frank Lampard

Frank Lampard akisherehekea bao lake

Frank Lampard, amedhihirisha kuwa bado angali mmoja wa wachezaji nyota wa soka hapa England, pale alipoingoza Chelsea, kuilaza Everton kwa magoli 2-1.

Ushindi huo ni wa tatu mfululizo kwa vijana hao wa Rafael Banitez.

Lampard ambaye kandarasi yake na Chelsea inakamilika mwisho wa msimu huu alifunga bao la kwanza kwa kicha pale alipopewa pasi safi na Ramires.

Everton ndio iliyokuwa wa kwanza kufunga kunako dakika ya pili ya mechi hiyo kupitia kwa nyota wake Steven Pienaar.

Baada ya Lampard, kuzawazisha Everton, walifanya mashambulio kadhaa hatari kwenye lango la Chelsea, lakini juhudi zao hazikuzaa matunda.

Mikwaju ya Victor Anichebe na Nikica Jelavic ziligonga mlingoti na hivyo kuinyima Everton ushindi katika uwanja wao wa Nyumbai.

Je Lampard atauzwa mwaka ujao?

Chelsea ilipata bao lake la pili kupitia kwa Lampard kunao kipindi cha pili.

Licha ya kufunga magoli hayo, kuna uwezekano mkubwa wa Lampard kutokamilisha msimu huu na Chelsea, kwa kuwa mkataba wake unamruhusu kuanzisha mazungumzo na klabu yoyote mwezi ujao.

Lakini mashambiki wengi wa Chelsea, wanahisi ni mapema kwa Lampard kuuzwa licha ya umri wake na pia kuwepo kwa wachezaji kama vile Oscar, Eden na Juan Mata.

Lampard alijiunga na Chelsea zaidi ya miaka kumi na moja iliyopita na amekuwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa sana.

Magoli ya Lampard yalisitisha rekodi ya Everton ya kutoshindwa katika uwanja wao wa nyumbani, uliokuwa umedumu kwa zaidi ya mechi kumi na nne.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.