Cole kujiunga na West Ham

Imebadilishwa: 3 Januari, 2013 - Saa 19:04 GMT

Joe Cole

Mcheza kiungo wa Liverpool Joe Cole anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake hadi klabu ya West Ham, kabla ya mechi ya kuwania kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Upton park.

Cole mwenye umri wa miaka 31, alifanyiwa uchunguzi wa matibabu hii leo na anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Cole amejiunga na West Ham, baada ya mcheza kiungo mwengine wa West Ham Yossi Benayoun, kujiunga na klabu ya Chelsea.

Usajili huo ni sharti uthibitishwa kabla ya saa tisa kamili majira ya Afrika Mashariki siku ya Ijumaa ili aweze kushiriki katika mechi hiyo ya siku ya jumamosi, dhidi ya Manchester United.

Cole hajaonyesha mchezo wa kuvutia tangu alipojiunga na Liverpool kutoka Chelsea mwaka wa 2010.

Msimu uliopita mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England aliichezea klabu ya Lille inayoshiriki katika ligi kuu ya Ufaransa kwa mkopo.

Uhamisho huo wa kujiunga na West Ham, huenda ukawa wa kudumu kwa sababu klabu hiyo ya London, tayari ina mchezaji mmoja wa Liverpool ambaye anaichezea kwa mkopo, Andy Carol.

Sheria za FA zinazuia vilabu kuwa na wachezaji wawili waliosajiliwa kwa mkopo kutoka kwa klabu mmoja.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.