RVP ainusuru Manchester United

Imebadilishwa: 6 Januari, 2013 - Saa 12:59 GMT
Robin van Persie

Robin van Persie akisherehekea bao lake

Robin van Persi alifunga bao dakika za mwisho na kuisaidia Manchester United kusalia kwenye kombe la FA, kwa ncha na kuinyima West Ham ushindi ambao ungelikuwa mkubwa zaidi kwa klabu hiyo mwaka huu.

Tom Cleverley aliifungia Manchester United bao lake la kwanza kabla ya James Collins kusawzisha kwa kichwa bao ambalo pia lilikuwa la kwanza tangu aliporejea tena kuichezea West Ham.

Collins alirejea tena kwa vishindo na kufunga bao la pili na kuwapa vijana hao wa West Ham uongozi wa magoli mawili kwa moja muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza.

Huku ikiwa imesalia sekunde chache kabla ya mechi kumalizika, wa mashabiki wa West Ham wakiwa wanashangilia ushindi wao dhidi ya Manchester United, nyota wa United Van Persie, aliwanyamazisha mashabiki hao kwa kuifungia United bao lake la pili.

United sasa itachuana tena na West Ham ili kuamua atakayejiunga na vilabu vingine katika raundi ijayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.