Messi ashinda tuzo ya Ballon d'Or

Imebadilishwa: 7 Januari, 2013 - Saa 19:46 GMT

Lionell Messi

Mshambulizi wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa nne mfululizo.

Messi, 25, alifunga jumla ya magoli 91 mwaka wa 2012 na aliwashinda wachezaji wengine Andres Iniesta wa Barcelona na Christiano Ronaldo wa Real Madrid.

Licha ya kufunga idadi hiyo ya magoli, timu yake ya Barcelona haikunyakuwa kombe la ligi kuu ya Uhispania ay kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka uliopita.

Abby Wambach, alishinda tuzo kwa upande wa kina dada naye Vicente del Bosque, akituzwa kuwa kocha bora.

Timu bora ya kwana ilijumuisha wachezaji wanaoshiriki katika ligi ya Uhispania pekee.

Messi alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo ya the Ballon d'Or, tuzo ambayo hukabithiwa mchezaji bora wa mwaka katika sherehe iliyofanyika mjini Zurich

Messi alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu walioteuliwa na jopo la wandishi wa habari na makocha wa timu za taifa, manaodha wa timu hiyo wakiwa ni pamoja na Iniesta na Ronaldo.

Mesi sasa ni mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda tuzo hiyo ya Ballons d'Or, kwa miaka minne mfululizo, rekodi anayoshikilia na aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa na rais wa UEFA kwa sasa Michel Platini.

Kikosi cha wachezaji bora wa mwaka 2012

•Iker Casillas (Real Madrid)
•Dani Alves (Barcelona)
•Gerard Pique (Barcelona)
•Sergio Ramos (Real Madrid)
•Marcelo (Real Madrid)
•Andres Iniesta (Barcelona)
•Xabi Alonso (Real Madrid)
•Xavi (Barcelona)
•Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
•Radamel Falcao (Atletico Madrid)
•Lionel Messi (Barcelona)

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.