Kocha wa Liverpool amtetea Suarez

Imebadilishwa: 7 Januari, 2013 - Saa 15:32 GMT
Luiz Suarez

Luiz Suarez akiunawa mpira

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema sio wajibu wa mshambulizi wake Luis Suarez kukiri aliunawa mpira wakati alipoifungia Liverpool bao lake la pili, wakati wa mechi ya raundi ya tatu ya kuwania kombe la FA dhidi ya Mansfeild.

Liverpool ilishinda mechi hiyo kwa magoli mawili kwa moja.

Wachezaji wa Mansfeild walilalamika kwa refa wa mechi hiyo, baada ya Suarez kuunawa mpira na kisha kufunga bao.

Alipoulizwa ikiwa Suareza anapaswa kukiri kuwa aliunawa mpira huo, Roggers alisema hilo sio jukumu lake kwa kuwa uamuzi wote unategemea refa.

'' Tukio hilo halikudhamiriwa, ilikuwa ni bahati mbaya tu, kwa hivyo ni wajibu wa refa wa mechi hiyo kuamua ikiwa Suarez aliunawa mpira au la'' alisema Roggers.

Wakati wa mechi hiyo, Daniel Sturridge aliyesajiliwa hivi majuzu na klabu hiyo alionyesha mchezo mzuri.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alisajiliwa kutoka kwa klabu ya Chelsea mwisho wa juma lililopita, na aliingia kama mchezaji wa ziada wakati wa mechi hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.