Kikosi cha Super Eagles kimetajwa

Imebadilishwa: 10 Januari, 2013 - Saa 17:50 GMT

Timu ya Taifa ya Nigeria

Nigeria imejumuisha wachezaji sita wanaocheza ligi ya nyumabani katika kikosi chake kitakachoshiriki katika fainali za kombe la Mataifa ya Afrika, idadi ambayo ndio kubwa zaidi kwa zaidi ya miongo miwili.

Mshambulizi anayecheza soka ya kulipwa nchini Marekani Bright Dike na mcheza kiungo Raheem Lawal, ambaye anayecheza nchini Uturukki wameachwa nje ya kikosi hicho.

Naodha Joseph Yobo, atashiriki katika fainali hizo kwa mara ya sita na mwisho.

Kikosi hicho cha Super Eagles pia kinajumuisha wacheza wa Chelsea Victor Moses na John Mikel Obi.

Siku ya Jumatano, mabingwa hao mara mbili wa kombe hilo, walitoka sare ya kutofungana bao lolote la Cape Verde ambayo inashiriki katika fainali hizo kwa mara kwanza, katika mechi ya kirafiki iliyochezwa nchini Ureno.

Kocha wa Nigeria Stephen Keshi, amesema bado ana wakati wa kutosha kuandaa kikosi chake.

Super Eagles imepangiwa kucheza mechi yao ya mwisho ya kirafiki tarehe 16 mwezi juu mjini Faro, kabla ya kuelekea nchini Afrika.

Baada ya kukosa fainali za mwaka wa 2012, Nigeria itakuwa na kibarua kigumu kudhihirisha kuwa bado ni moja wa miamba wa soka barani Afrika.

Kikosi cha Nigeria

Walinda lango: Vincent Enyeama (Maccabi Tel Aviv, Israel), Austin Ejide (Hapoel Be'er Sheva, Israel), Chigozie Agbim (Enugu Rangers)

Walinzi:

Elderson Echiejile (SC Braga, Ureno), Juwon Oshaniwa (Ashdod FC, Israel), Joseph Yobo (Fenerbahce, Uturuki), Efe Ambrose (Celtic, Scotland), Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves), Kenneth Omeruo (ADO Den Haag, Uholanzi), Godfrey Oboabona (Sunshine Stars)

Wacheza kiungo:

John Mikel Obi (Chelsea, England), Nosa Igiebor (Real Betis, Uhispania), Ogenyi Onazi ( Lazio, Italia), Obiora Nwankwo (Padova, Italia), Fegor Ogude (Valerenga, Norway), Gabriel Reuben (Kano Pillars)

Washambulizi:

Ahmed Musa ( CSKA Moscow, Urussi), Emmanuel Emenike (Spartak Moscow,Urussi), Victor Moses (Chelsea, England), Sunday Mba (Enugu Rangers), Ikechukwu Uche (Villarreal, Uhispania), Brown Ideye (Dynamo Kiev, Ukraine), Ejike Uzoenyi (Enugu Rangers)

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.