Liverpool yaambulia patupu Old Trafford

Imebadilishwa: 13 Januari, 2013 - Saa 19:04 GMT

Robin van Persie akisherehekea bao lake

Manchester United, imeendeleza uongozi wake katika msururu wa ligi kuu ya Premier ya England baada ya kuilaza Liverpool kwa magoli mawili kwa moja, katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford.

Nyota wa Manchester United, Robbin Van Persie, ndiye aliyeifungia United bao lake la Kwanza.

Katika kipindi cha pili mcheza kiungo wa Manchester United, Patrice Evra akaongeza bao la pili na hivyo kudidimiza matumainio ya Liverpool ya kuandikisha ushindi wao kwa kwanza katika uwanja huo kwa zaidi ya miaka mitano.

Mchezaji wa ziada wa Liverpool, Daniel Sturridge ambaye alisajili hivi majuzi kutoka kwa klabu ya Chelsea alifufua matumaini ya Liverpool kwa kufunga bao moja.

Licha ya Liverpool kuimarika katika kipindi hicho cha pili mechi hiyo ilimalizika Manchester United 2 Liverpool 1.

Kufuatia ushindi huo, Manchester United ingali kileleni mwa ligi hiyo na alama 55, alama saba nyuma ya mahasimu wao wa karibu Manchester City.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.