Arsenal kucheza na Swansea katika kombe la FA

Imebadilishwa: 16 Januari, 2013 - Saa 13:12 GMT

Kocha wa Arsenal Arsen Wenger

Arsenal inashuka uwanjani leo usiku bila wachezaji wake Laurent Koscielny na Mikel Arteta, kwa mechi ya raundi ya tatu ya kuwania kombe la FA dhidi ya Swansea, katika uwanja wa Emirates.

Mlinda lango Koscielny, hatacheza baada ya kupewa kadi nyekundi kati mechi iliyopita naye mcheza kiungo Arteta anauguza jeraha la mguu.

Hata hivyo masaibu ya Arsenal huenda yakajibiwa na kurejea kwa Abou Diaby ambaye alikosa mechi ya ligi dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili.

Na kama ilivyokuwa wiki mbili zilizopita, kocha wa Swansea Michael Laudrup, hana matatizo yoyote ya majeruhi.

Hata hivyo hatamshirikisha mechaji wake aliyesajiliwa hivi majuzu mwa mkopo Roland Lamah, kwa sababu jina lake halikuwasilishwa kwa muda ufaao.

Ikiwa Swansea itafuzu kwa raundi ya nne ya kombe hilo kwa msimu wa tatu mfululizo, itahitaji kuiondoa timu inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Premier, hatua ambayo haijaafikiwa tangu ilipoiondoa Portsmouth katika rauni ya nne miaka minne iliyopita.

Kwa sasa, ina alama tatu nyuma ya Arsenal inayoshikilia nafasi ya sita kwenye msururu wa ligi kuu na katika kombe la ligi, iliilaza Chelsea magoli mawili kwa bila katika raundi ya kwanza ya nusu fainali.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.