Guardiola aelezea nia ya kwenda England

Imebadilishwa: 16 Januari, 2013 - Saa 14:20 GMT
Pep Guardiola

Pep Guardiola

Aliyekuwa kocha wa Barcelona, Pep Guardiola, amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu azma yake ya kuongoza timu inayoshiriki kweny ligi kuu ya England.

Guardiola, ambaye aliongoza Barcelona kushinda tuzo kumi na nne katika kipindi cha miaka minne, kwa sasa anatarafuta kazi.

Matamshi yake sasa yatayasisimua vilabu vya Manchester City, Chelsea na Manchester United, ambavyo vinaaminika kuwa vimekuwa vikifuatilia hali ya kocha huyo wa zamani wa Barcelona.

Tangazo hilo limetolewa, baaday kocha wa Real Madrid Jose Mourinho kuelezea nia na azma yake ya kutaka kurejea Uingereza, wakati kandarasi yake itakapokamilika.

Ni anataka Uingereza?

Pep Guardiola baada ya kushinda ligi kuu nchini Uhispania

Guardiola amesema ni jambo la fahari kushiriki katika ligi kuu ya Premier ya England.

Kocha huyo kwa sasa anaishi mjini New York na familia yake, baada ya kuamua kuchukua likizo ya mwaka mmoja, kutoka kwa masuala yote ya mchezo wa soka.

Lakini akiongea katika sherehe za kutuza mchezaji bora wa mwaka wa shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, mapema mwezi huu, Guardiolaa, alithibitisha kuwa atarejea tena katika msimu wa mwaka wa 2013-14.

Vilabu vya Bayern Munich na AC Milan pia vimehusihswa na kocha huyo ambaye alijiuzulu kama kocha wa Barcelona mwaka wa 2012.

Wasifu wa Pep Guardiola

  • Alizaliwa Janurari 18, 1971 nchini Uhispania.
  • Aliichezea vilabu vya Barcelona B (1990-92), Barcelona (1990-2001), Brescia (2001-02), Roma (2002-03), Brescia (2003), Al-Ahli (2003-05), Dorados (2005-06), Spain (1992-2001).
  • Aliichezea timu ya taifa ya Uhispania mechi 47.
  • Amezifunza vilabu vya Barcelona B (2007-08), Barcelona (2008-2012)
  • Ameshinda tuzo tatu z aligi kuu ya premier, tatu za Supercopa de Espana titles, mbili za Copa Del Rey titles, mbili za kombe la klbau bingwa barani ulaya mbili za kom la Uefa na mbili za kombe la klabu bingwa duniani.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.