Kocha wa Afrika Kusini awashutumu wachezaji

Imebadilishwa: 22 Januari, 2013 - Saa 12:41 GMT

Gordon Igesund

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini, Gordon Igesund, amewashutumu wachezaji wake kwa kukosa umakini, baada ya timu hiyo ya Bafana Bafana kutoka sare ya kutofungana bao lolote na Cape Verde, katika mechi yao ya ufunguzi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Afrika Kusini.

Igesund, ambaye ni kocha wa tatu kuliongoza Bafana Bafana, tangu mwaka wa 2010, alikiri kuwa wachezaji wake walionyesha mchezo mbaya katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Soccer City, mjini Johannesburg.

Igesund amesema alihisi wachezaji wake walikuwa na uoga mwingi wakati wa mechi hiyo kwa sababu wengi wao hawakucheza kama alivyotarajia katika kipindi cha kwanza.

Cape Verde, ambayo ni nchi ndogo zaidi barani Afrika, inashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza na iliwashangaza wengi pale ilipoonyesha mchezo mzuri kuliko wenyeji wao Afrika Kusini.

Timu ya Taifa ya Cape Verde

Cape Verde nusura iifunge Bafana Bafana wakati mcheza kiungoi Babanco alipomuandalia pasi nzuri Platini, ambaye naye akaupiga kombora ambalo lilikosa lango na Afrika Kusini kwa ncha.

'' Wacheza viungo wetu hawakushirikiana vyema na washambulizi wetu na mara nyingi tulionekana kuwapa washambulizi mipira kama hawako tayari'' Alisema kocha huyo wa Afrika Kusini.

Kocha wa Cape Verde Lucio Antunes, kwa upande wake alisema kuwa ameridhisha na matokeo ya mechi hiyo na kuwa wachezaji wake wameiletea taifa lao sifa na heshima kuu.

'' Nia yetu sasa ni kuangazi mechi zilizosalia za makundi, kwa kuwa matarajio yetu ni kufuzu kwa raundi ijayo, na baada ya mechi yetu ya kwanza na Afrika Kusini, nahisi tuna nafasi nzuri'' Alisema Antunes.

''Kama taifa tumefurahishwa sana na matokeo yeti. Ni taifa la watu laki tano, lakini matokeo yetu yatawafurahishwa na kwa sasa hatuna cha kuogopa katika mechi zilizosalia''

Afrika Kusini imeratibiwa kucheza Angola katika mechi yake ya pile nayo Cape Verde kucheza na Morocco.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.