Afrika Kusini 2 Angola 0

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 16:30 GMT

Mchezaji wa Angola Manucho

Afrika Kusini imeanza mechi yake ya pili ya kombe la mataifa ya Afrika,vyema kuliko ilivyocheza katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Cape Verde.

Wenyeji katika kipindi cha kwanza Bafana Bafana ilifanya mashambulio kadhaa katika lango la Angola.

Mshambulizi matata wa Angola, Manucho ambaye anaiongoza kikosi hicho katika fainali hizo kwa mara nyingine analindwa na mabeki wawili wa Afrika Kusini na juhudi zake za kupenya zimeambulia patupi.,

Kunako dakika ya kumi na tano Afrika Nusuru ifunga bao lakini msaidizi wa refa wa mechi hiyo aliinua kijibendera kuashiria kuwa alikuwa ameotea.

Dakika mbili baadaye Bafana Bafana ilifanya shambulio lingine la mkwaju wa Siyabonga Sangwen ulikosa gola kwa ncha.

Kunako dakika ya 30 Siyabonga Sangweni aliifungia Afrika Kusini bao lake la kwanza.

Baada ya dakika 45 za kwanza, Angola wanajikuta katika njia panda ila kocha wake ana farahi kuwa wamefungwa bao moja pekee licha ya mashambulio hatari kama matano hivi, yaliyofanywa na Afrika Kusini.

Mechi itakayofuatia itakuwa kati ya Morocco na Cape Verde.

Kipindi cha pili kilianza huku Angola ikiwa na wachezaji kumi pekee baada ya refa wa mechi hiyo kuanza mpira kabla ya kuruhusu mabadiliko katika kikosi cha Angola.

Kinyume na iliyokuwa katika kipindi cha kwanza wachezaji wa Angola walianza kuonana na kufanya mashambulio kadhaa katika lango la Afrika Kusini.

Licha ya juhudi hizo za Angola, Afrika Kusini ilipata bao lake la pili kunako dakika ya 61 kupitia kwa mchezaji wake wa ziada Lehlohonolo Majoro ambaye alikuwa ameingia uwanjani dakika mbili tu kabla ya kufunga bao hilo.

Dadika ya 70 Afrika Kusini 2 Angola 0

Kikosi cha Angola

Kikosi cha Afrika Kusini

01 Lama

03 Lunguinha

04 Massunguna

13 Bastos

15 Miguel

06 Dede

16 Pirolito

18 Da Costa

09 Manucho

17 Mateus

23 Afonso

Wachezaji wa Ziada

12 Landu

22 Neblu

02 Airosa

05 Fabricio

10 Zuela

14 Costa

20 Mingo Bile

07 Djalma

08 Dinis

11 Gilberto

16 Khune

03 Masilela

05 Ngcongca

13 Khumalo

21 Sangweni

15 Furman

18 Thuso Phala

19 Mahlangu

09 Mphela

17 Parker

23 Rantie

Wachezaji wa Ziada

01 Sandilands

22 Meyiwa

02 Gaxa

04 Nthethe

11 Matlaba

08 Tshabalala

10 Serero

12 Letsholonyane

20 Manyisa

07 Majoro

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.