Nani atatamba kati ya Mali na Ghana?

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 18:58 GMT

Timu ya Taifa ya Ghaba

Baada ya timu za kundi A kucheza mchezo wa pili kila moja, kesho ni kindumbwendubwe cha kundi B.

Vinara wa kundi hilo Mali itakuwa ikipepetana na Ghana, huku miamba ya kutoka misitu ya kati ya Afrika, DR Congo wataonyeshana kazi na Niger.

Mpaka sasa Mali ndiyo inayoongoza kundi hili kwa kujikusanyia pointi tau baada ya kuilaza Niger katika mechi yao ya kwanza, huku Ghana na DR Congo zote zina pointi moja moja kila moja.

Mali ndio watakaoanza kuchachafyana na Ghana, huku mechi ya pili ikiwakutanisha DR Congo na Niger itakayokuwa ikiwania pointi tatu kwani ikipoteza katika mchezo huo tayari itakuwa imechimbia kaburi, kutokana na kutokuwa na pointi hata moja.

Kikosi cha DRC

Timu zote zina nafasi ya kusonga hatua ya robo fainali iwapo zitachanga vizuri karata zao.

Katika kundi A, Afrika Kusini inaongoza ikiwa na pointi nne na kufuatiwa na Cape Verde na Morocco zenye pointi mbili kila mmoja.

Afrika Kusini itakayopambana na Morocco itahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya robo fainali, huku Cape Verde, Morocco na Angola zote zikihitaji ushindi katika mechi zao za mwisho.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.