DRC 0 Niger 0

Imebadilishwa: 24 Januari, 2013 - Saa 17:50 GMT

DRC ikicheza na Ghana

Niger hatimaye imepata pointi ya kwanza katika michuano ya Kombe la Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini, baada ya kutoka sare ya kutofungana bao lolote na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mchezajiwa DRC akikabiliana na mwenzake wa Niger

Katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Mali, Niger iliweza kuwabana Mali kwa dakika 84 kabla ya kukubali kipigo cha goli 1-0 kufuatia goli lililofungwa na Seydou Keita.

Katika kipindi cha kwanza Niger ilionekana kuilemea Congo na ilifanya mashambulizi kadhaa katika lango lao.

Kipa wa DRC, Kidiaba hata hivyo alifanya makosa kadhaa ambayo nusura yaipe Niger uongozi.

Modibo Sidibe alimpokonya mpira mcheza kiungo wa DRC, ila mkwaju wake ukagonga mlingoti kunako dakika ya tano ya mechi hiyo.

Daouda Kassaly ambaye alisababisha Niger kushindwa mechi yao ya ufunguzi katika mchezo huu alioonyesha mchezo mzuri kwa kuokoa mkwaju uliopigwa na mshambulizi wa DRC Dieumerci Mbokani.

Juhudi za mchezaji wa West Brom Youssouf Mulumbu za kufunga wakati wa mechi hiyo hazikufua dafu pale alipodhibitiwa vikali na walinda lango wa Niger, katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Port Elizabeth.

Mashabiki wa Niger

Baada ya dakika 45 za kwanza hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzie.

Kinyume na ilivyotarajiwa Tresor Mputu, hakucheza kadri ya uwezo wake na kocha wa DRC, LeRoy, alimuondoa katika kipindi cha pili na mahala pake kuchukuliwa na Zola Matumona.

Kocha huyo pia alimuondoa mcheza kiungo Patou Kabangu na kumweka mshambulizi Dioko Kaluyituka.

Baada ya mabadiliko hayo, kikosi hicho cha Congo kilionekana kuimarika na kikaanza kufanya mashambulio katika lango la Niger.

Congo ingeliibuka na ushindi katika mechi hiyo endapo wachezaji wake wangelikuwa makini katika kumalizia.

Kunako muda wa ziada, Niger ilifanya shambulio moja hatari katika lango la DRC, lakini mkwaju wa Karim Lancina uliokolewa na kipa wa Congo, Kidiaba.

Hata hivyo mechi hiyo imemalizika huku timu hizo mbili zikigawana alama moja kila mmoja.

Ghana sasa inaongoza kundi hilo kwa alama nne ikifuatiwa na Mali yenye alama 3, DRC ikiwa ya tatu na alama mbili na Niger ikivuta mkia na alama moja.

DRC sasa ni sharti ishinde mechi yake ya mwisho dhidi ya Mali na iombe Niger ishindwe na Ghana ili ifuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

Kikosi cha Niger

Kikosi cha DRC

6 Daouda
08 Kourouma
13 Chicoto
18 Dan Kowa
19 Koudize
21 Bachar
23 Soumaila
03 Lancina
14 Issoufou
02 Maazou
07 Sidibe

Wachezaji wa Akiba:

01 Alzouma
22 Saminou
04 Amadou
05 James
15 Alassane
06 Laouali
10 Talatou
12 Sakou
17 N'Gounou
20 Amadou
09 Kamilou
11 Issoufou

01 Kidiaba
02 Issama
03 Kasusula
05 Mabiala
17 Mongongu
07 Mulumbu
18 Makiadi
04 Kabangu
08 Mabi
09 Mbokani
15 LuaLua

Wachezaji wa Akiba:

16 Mandanda
23 Bakala
19 Mbemba
21 Zakuani
10 Matumona
12 Ilunga
22 Kisombe
06 Manzia
11 Kanda
13 Kaluyituka
20 Luvumbu

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.