Kati ya Zambia na Nigeria nani Jogoo?

Imebadilishwa: 24 Januari, 2013 - Saa 20:13 GMT

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kuendelea kesho na mabingwa watetezi Zambia watakabilina vilivyo na Nigeria.

Kundi C linaingia katika mzunguko wa pili ambapo Zambia imeratibiwa kucheza na Super Eagles ya Nigeria.

Tofauti na sasa zinapokutana katika hatua ya mzunguko wa pili wa mechi za kundi C, timu hizo zitakuwa zikirejea historia ya fainali za mwaka 1994, nchini Tunisia, ambapo zipambana na Nigeria kuibuka mabingwa.

Hii itakuwa ni mechi ya kwanza kwa timu za kundi C, katika mzunguko wa pili na mechi itakayofuata ya kundi hilo Burkina Faso itapambana na Ethiopia.

Wachezaji wa Zambai wakati wa mechi yao na Ethiopia

Mpaka sasa kundi hilo halitabiriki kutokana na ubora wa vikosi vyao. Timu zote nne zina pointi moja moja, baada ya kutoka sare.

Kwa mtazamo huo kila moja itakuwa ikipigania kupata pointi tatu muhimu, kwa maana kila moja ina nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali iwapo itachanga vizuri karata zake.

Kwa matarajio ya mamilioni ya mashabiki walio nyuma yake, kocha wa Nigeria Stephen Keshi, sasa angalau mzigo umepungua baada ya kufika mchezaji wa Chelsea Victor Moses kabla ya kuvaana na Zambia hapo kesho katika michuano hiyo ya Kombe la Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Keshi amezungumza siku ya Alhamisi kuhusu ugumu unaomkabili katika kuongoza kikosi cha Nigeria, ambacho mashabiki wake wana matarajio makubwa ya kuibuka mabingwa licha ya kutofanikiwa kutwaa taji hilo la Afrika tangu mwaka 1994.

Ushindi huo ulikuja wakati Nigeria ilipokuwa katika kiwango bora zaidi cha soka barani Afrika, hali iliyosababisha nchi hiyo kushindana katika hatua za juu za kuwania vikombe katika mashindano mbalimbali ya soka duniani.

Chipolopolo yaapa kutokomeza Euper Eagles

Keshi, ambaye alikuwa nahodha mwaka 1994, wakati The Eagles waliptwaa ubingwa wa Afrika, ana matumaini ya kurejea historia hiyo, na kumkaribisha Moses baada ya mchezaji huyo wa Chelsea kukosa mechi ya kwanza dhidi ya Burkina Faso siku ya Jumatatu.

Wachezaji wa Nigeria

Mechi hiyo iliishia kwa sare ya 1-1.

Keshi alikuwa nahodha wa Nigeria wakati wa fainali za Kombe la Afrika zilizofanyika Tunisia, ambapo waliibwaga Zambia katika mechi ya fainali kwa mabao 2-1.

Zambia katika fainali hizo iliundwa na kikosi kipya kabisa cha wachezaji baada ya wachezaji wote waliokuwa katika ndege kufa katika ajali ya ndege hiyo pwani ya Gabon wakielekea Tunisia.

Kalusha Bwalya ambaye alikuwa nahodha wa Zambia, wakati huo ikijulikana kama KK,alinusurika kutokana na kutokuwemo katika ndege hiyo. Sasa Kalusha Bwalya ni rais wa Shirikisho la Soka la Zambia.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.