Zaha kusaini mkataba na Man United

Imebadilishwa: 24 Januari, 2013 - Saa 19:15 GMT

Winfred Zaha

Winfred Zaha anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa matibabu katika klabu ya Manchester United siku chache zijazo kabla ya uhamisho wake kukamilika kutoka kwa klabu ya Cyrstal Palace.

Ripoti zinasema United imelipa kitita cha pauni milioni 15 kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye alijiunga na Crystal palace akiwa na umri wa miaka kumi na miwili.

Zaha amesaini mkataba wa miaka mitano na Manchester United na anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza na timu ya taifa ya Uingereza mwezi ujao.

Awali kulikuwa na ripoti kuwa Crystal Palace haikuwa na nia ya kumuuza mchezaji huyo lakini, inaonekana kuwa mazungumzo kati ya kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson na wasimamizi wa klabu hiyo yalizaa matunda.

Sir Alex Ferguson alisalia nyuma baada ya kikosi chake kuelekea nchini Qatar kwa mazoezi zaidi, ili kuendeleza mazungumzo kuhusu usajili wa mchezaji huyo.

Victor Wanyama

Kocha huyo pia alikwenda nchini Scotland kutizama mechi ya Celtic, ili kumchunguza mcheza kiungo wa Celtic, kutoka Kenya, Victor Wanyama.

Wanyama amekuwa nyota wa Celtic, katika michuano ya kuwania ko,be la klabu bingwa barani ulaya.

Wakati wa mechi hiyo Wanyama, aliifungia Celtic bao moja na ripoti zinasema kuwa vilabu vingine vikiwemo Arsenal, Tottenham na Liverpool vile vile vinamsaka mchezaji huyo kutoka Kenya.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.