Ethiopia kuchuana na Burkina Faso

Imebadilishwa: 25 Januari, 2013 - Saa 17:30 GMT

Mchezaji wa Ethiopia Adame Girma

Burkina Faso, imemjumuisha mcheza kiungo wa Marseille, Charles Kabore, katika kikosi cha wachezaji wake wa kwanza katika mechi yao ya pili ya kundi C dhidi ya Ethiopia.

Kufikia sasa Tunisia inaongoza kwa bao moja kwa bila bao amablo lilifungwa kunako dakika ya 34 kupitia kwa mchezaji Alain Traore.

Awali kocha wa Ethiopia, Sewnet Bishaw, amefanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake.

Kipa wake kwa kwanza Jemal Tassew, atakosa mechi ya leo baada ya kupewa kadi nyekundi wakati wa mechi yao na Zambia.

Kocha wa Burkina Faso, anasema wanaliheshimu sana kikosi cha Ethiopia, ambacho kimekuwa kikiimarika kila uchao.

Mchezaji wa Burkina Faso

Ethiopia ilitoka sare mechi yao ya ufunguzi dhidi ya mabingwa watetezi Zambia, licha ya kucheza wakiwa wachezaji kumi pekee kwa zaidi ya dakika sitini za mechi hiyo.

Kocha wa Ethiopia Sewnet Bishaw, kwa upande wake, amesema memchi yao na Zambia, iliwapo uzoevu mkubwa hasa kutokana na sababu kuwa hawajawahi kucheza na timu hizo kwa zaidi ya miaka thelathini na moja.

Bishaw, amesema wachezaji wake wako katika hali nzuri na anatarajia matokeo mema katika mechi hiyo.

Ameongeza kusema kuwa nia yao kuwa ni kufuzu kwa raundi ijayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.