Algeria kupambana na Togo

Imebadilishwa: 26 Januari, 2013 - Saa 13:29 GMT

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Togo

Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amesema atafanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake kitakachopambana na Togo, katika mechi yao ya pili ya michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini ili kuimarisha matumaini yao ya kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

Algeria hata hivyo huenda ikakosa huduma za nyota wake Sofiane Feghouli, ambaye alijeruhiwa wakati wa mechi ya siku ya Jumanne dhidi ya Tunisia.

Wachezaji wa Algeria

Algeria ilipoteza mechi hiyo ya ufunguzi na sasa ni sharti ishinde mechi ya leo ili iwe na nafasi ya kusonga mbele.

Togo, kwa upande wake, haina matatizo yoyote ya majeraha na huenda kikosi kilichocheza mechi yao ya kwanza ndicho kitakachocheza hii leo.

Kundi D imetajwa kundi la mauti

Magwiji hao kutoka Magharibi mwa Afrika nao wanahitaji ushindi katika mechi ya leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupiga hatua, katika mashindano hayo.

Emmanuel Adebayor

Togo ilipoteza mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Ivory Coast ambayo hii leo inacheza na Tunisia.

Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amesema, wamejifunza mengi kutokana na mechi yao ya kwanza na kwa sasa vijana wake na ari ya kushinda ila amekiri kuwa mechi ya leo sawa na mechi ya ufunguzi itakuwa ngumu.

Mkufunzi wa Togo Didier Six naye amesema walifanya mkutano wa dharura baada ya mechi yao ya kwanza ili kujadili yale yaliyokwenda mrama na kupanga mikakati ya kujiimarisha katika mechi zilizosalia za makundi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.