Afrika Kusini yasonga mbele

Imebadilishwa: 27 Januari, 2013 - Saa 19:23 GMT

Kikosi cha Afrika Kusini

Afrika Kusini, wenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, imefuzu kucheza hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya 2-2 na Morocco.

Kwa matokeo hayo Afrika Kusini inaongoza kundi A ikiwa na pointi 5 sawa na Cape Verde, lakini ikiizidi kwa wingi wa magoli.

Katika mchezo wa leo Morocco ndiyo iliyoanza kufunga katika dakika ya kumi ya mchezo, likitiwa kimiani na El Adoua.

Matokeo hayo yaliyodumu hadi mapumziko.

Huku Morocco ikiamini kuwa imeshinda, ilishtukia Afrika Kusini wanasawazisha katika dakika ya 71 kupitia kwa Mahlangu.

Morocco haikukata tamaa kusaka ushindi, na iliwezakutia kimiani goli la pili katika dakika ya 82, mfungaji akiwa Abdelilah Elhafidi.

Kocha wa Morocco

Furaha ya Morocco ilidumu kwa dakika nne tu, kwani katika dakika ya 86, Afrika Kusini kupitia kwa mshambuliaji wake Rantie, walisawazisha na kukata tikiti ya kucheza robo fainali.

Afrika Kusini na Cape Verde ndizo zilizofuzu katika kundi A kucheza hatua ya robo fainali.

Morocco yenye pointi 3 na Angola yenye pointi 1 kutoka kundi A, zimeiaga michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2013.

Kundi B kesho litakuwa linakamilisha michezo yake, kwa Ghana kumenyana na Niger, huku DR Congo ikipepetana na Mali.Mpaka sasa Ghana ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi 4, ikifuatiwa na Mali pointi 3, DR Congo pointi 2 na Niger imeweka kibindoni pointi 1.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.