Djokovic atwaa taji la Australian Open

Imebadilishwa: 27 Januari, 2013 - Saa 17:56 GMT

Novak Djokovic akishangilia ubingwa wa Australian Open

Katika mashindano ya Tennis mchezaji nambari moja duniani Novak Djokovic, leo ameshinda taji la la nne katika mashindano ya tennis ya Australia Open pale alipomuangusha Andy Murray, katika fainali.

Mchezaji huyo kutoka Serbia, alitumia muda wa saa tatu na dakika arobaini kumshinda Murray kwa seti tatu kwa moja za 6-7 7-6 6-3 na 6-2.

Andy Murray akiokoa moja ya mipira

Hata hivyo juhudi za Murray za kushinda kombe hilo mwaka huu, ziliingia kasoro baada ya kupata jeraha la mguu, ambalo lilimfanya kushindwa kukabiliana na mpinzani wake.

Kufuatia ushindi huo, Djokovic sasa ameshinda mataji sita katika mashindano ya tennis ya Grand slam na kuandikisha historia ya kuwa mtu wa kwanza kuwahi kushinda fainali za mashindano hayo ya Australia kwa miaka mitatu mfululizo, tangu miaka arobaini na sita iliyopita.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.