Leroy Fer asajiliwa na Everton

Imebadilishwa: 28 Januari, 2013 - Saa 15:23 GMT

Leroy Fer

Everton imekubali kulipa kitita cha puani milioni saba kumsajili mcheza kiungo wa FC Twente, kutoka Uholanzi Leroy Fer.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amefunga magoli kumi baada ya kucheza mechi ishirini na tisa kwa klabu hiyo ya FC Twente chini ya Kocha Steve McClaren.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwa wavotu wa klabu hiyo, mchezaji huyo sasa anatarajiwa kufika England kujadiliana kuhusu mshahara wake na pia kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Everton, ambayo inacheza na West Brom siku ya Jumatano inashikilia nafasi ya tano kwenye msururu wa ligi kuju ya Premier, alama tatu nyumba ya Tottenham.

Fer, ameichezea timu ya taifa ya Uholanzi mechi mbili na anajulikana kwa jina la utani "The Bouncer"kutokana na umbo lake.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.