DRC 1 Mali 1

Imebadilishwa: 28 Januari, 2013 - Saa 17:20 GMT

Timun ya Taifa ya Soka na DRC

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo inacheza mechi yao ya makundi ya michuaano ya kuwania kombe la mataia ya Afrika, dhidi ya Mali.

DRC ilipata bao lake kupitia kwaju wa penalti uliopigwa na Dieumerci Mbokani.

Lakini Mali ikajibu dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Mahamadou Samass.

Kufikia sasa DRC 1 Mali 1

Timu hizo mbili ni sharti ishined mechi hiyo ya Kundi B, ili ifuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

Endapo timu hizo mbili zitashona nguvu, Mali, huenda ikafuzu kwa robo fainali, ikiwa mechi nyingine ya Kundi hilo kati ya Niger, itamalizika huku timu hizo zikitoshana nguvu au Ghana ikiibuka na ushindi.

Timu ya taifa ya Mali

DRC, inashikilia nafasi ya tatu katika kundi hilo baada ya kutoka sare mechi zao mbili za kwanza.

Mali imefanya mabadiliko manne katika kikosi chake ambacho kilishindwa na Ghana.

Mlinda lango Molla Wague, mcheza kiungo Samba Sow na washambuliaji nMahamadou Samassa na Modibo Maiga wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji wa kwanza kumi na mmoja

Kocha wa Congo, Claude LeRoy, anasema kikosi chake kinakabiliwa na kibarua kigumu kuipiku Mali.

‘‘Ushindi pekee ndio utakaotuwezesha kufuzu kwa robo fainali’’ alisema LeRoy.

Ni timu hiyo ya Congo, pekee ndiyo iliyofuzu kwa fainali hizo mwaka huu, kutoka kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Hata hivyo makocha wa timu hizo mbili watakuwa na wachezaji wao wote katika mechi hiyo.

Kocha huyo wa Congo amesema amewahimiza wachezaji wake kucheza mchezo wa kushambuliaili kuimarisha nafasi yao.

Naye kocha wa Patrice Carteron, amesema nia yao kuu ni kutoka sare, ili kujihakikishia nafasi katka raundi ijayo na ni lazima tusahau, kipigo tulichopata dhidi ya Ghana na kuangazia mechi dhidi ya Congo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.