Balotelli asajiliwa na AC Millan

Image caption Mario Balotelli

Mkurugenzi wa klabu ya AC Millan, Umberto Gandini amethibitisha kuwa klabu hiyo imemsajili mshambuliaji wa Manchester City Mario Balotelli kwa mkataba wa miaka minne na nusu.

Balotelli, 22, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu mjini Milan siku ya Jumatano kabla ya kusaini wake na klabu hiyo.

Inakisiwa kuwa AC Milan imemsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 20.

Awali Manchester City ilianzisha mazungumzo na vilabu vya AC Milan na Juventus kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wake Mario Balotelli, na ripoti zinasema kuwa, Balotelli atauzwa ikiwa vilabu hivyo vitaweza kulipa fedha wanazo taka.

Klabu hiyo imesema mchezji huyo mwenye umri wa miaka 22, anakisiwa kugharibu pauni milioni ishirini na moja mbali na fedha zingine za ziada.

Balotelli hana haraka ya kuuzwa na Manchester City imesema haina mipango ya kupunguza mshahara wake ili aondoke.

Kinyume na matarajio ya wengi Balotelli amesafiri na wachezaji wa Manchester City watakaocheza na QPR katika mechi ya ligi kuu ya premir leo usiku.

Milan ilianzisha mazungumzo na Man City, kuhusu mchezaji huyo kutoka Italia na kuna ripoti kuwa klabu ya Juventus vile vile imewasilisha ombi la kutka kumsajili Balotelli, ambaye alijiunga na Manchester City Agosti mwaka wa 2010 kwa kitita cha pauni milioni 24.

Image caption Mario Balotelli akizozana na kocha wake

Mapema siku ya Jumatatu, naibu kocha mkuu wa Man City, David Platt, alisema kuwa Balotelli hatajiunga na AC Millan mwezi huu.

Siku ya Ijumaa wiki iliyopita, kocha wa Man City Roberto Mancini, alikariri hana nia ya kumuuza kuwa mchezaji huyo kutoka Italia.

Balotelli ambaye amefunga goli moja baada ya kucheza mechi kumi na nne msimu huu, amekumba na kashfa nyingi tangu aliposajiliwa.

Tukio la hivi karibuni, likiwa mzozo kati yake na Mancini katika uwanja wao wa mazoezi mwanzo wa mwezi huu.

Makamu wa rais wa AC Milan Adriano Galliani amesema ikiwa Manchester City itapunguza bei ya mchezaji huyo, basi huenda wakamsajili.