Nigeria imefuzu kwa robo fainali ya AFCON

Image caption Mashabiki wa Ethiopia

Nigeria inaelekea imefuzu kwa robo fainali ya michuano ya kuwania kombe la bingwa barani Afrika baada ya kuilaza Ethiopia kwa bao moja kwa bila katika mechi yao ya mwisho ya makundi.

Victor Moses aliifungia Nigeria bao hilo muhimu kunako dakika ya 79, kwa njia ya penalti.

Dakika mbili baadaye Nigeria ikapata bao la pili kupitia mkwaju mwingine wa penalti.

Sasay Bancha alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa wa Nigeria na hivyo kumlazimisha refa wa mechi hiyo kuumpa kadi ya pili ya njano.

Sawa na ilivyokuwa awali Victor Moses ndiye aliyetunukiwa jukumu hilo la kuupiga penalti na bila kukosea, akafunga la pili na kuhakikisha kuwa Nigeria inasonga mbele kwenye robo fainali ya mashindano hayo.

Super Eagles ilitoka sare mechi zake za kwanza mbili na hivyo ilihitaji shari ushindi mechi ya leo ili ifuzu kwa raundi ijayo yab mashindano hayo.