Ivory Coast 2 Algeria 2

Image caption Wachezaji wa Ivory Coast

Ivory Coast imemaliza mechi zake katika kundi D kwa kuongoza ikiwa na pointi saba.

Matokeo hayo yanafuatia mechi zake mbili za awali kwa kushinda zote dhidi ya Togo na Tunisia na kutoka sare ya 2-2 na Algeria katika mchezo wa mwisho.

Timu ya Ivory Coast ilikuwa ikikamisha ratiba na kutafuta nafasi katika kundi hilo kwani ilikuwa imekwisha fuzu kucheza robo fainali.

Image caption Mlinda mlango wa Togo

Algeria, nayo inacheza mechi hiyo, ikiwa na uhakika kuwa matokeo ya mechi hiyo hayatakuwa na maana kwao, baada ya kuyaaga mashindano hayo, kwani ilikuwa imepoteza michezo yote miwili ya awali.

Algeria ilipoteza mechi zake mbili dhidi ya Togo na Tunisia. Hata hivyo imeweza kuambulia pointi moja.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo D, Togo ilipambana na Tunisia mechi ambayo imemalizika kwa timu hizo kufungana goli 1-1.

Timu zilizofuzu kutoka kundi D ni Ivory Coast na Togo ambayo ilikuwa na pointti 4 kama Tunisia, lakini Tunisia ikidunishwa kwa kufungwa magoli mengi.