Ghana 2-Cape Verde 0

Image caption Mchezaji wa Ghana

Ghana yaingia nusu fainali baada ya kuicharaza Cape Verde 2-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali.

Ghana imepata bao la kwanza katika kipindi cha pili likifungwa na Mubarak Wakaso kwa njia ya penalti katika dakika ya 54.

Wakaso tena iliihakikishia Ghana kusonga mbele baada ya kufunga bao la pili katika dakika ya tisini.

Kwa matokeo hayo Cape Verde imeyaaga rasmi mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Hata hivyo Cape Verde ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza ilionyesha upinzani mkubwa na michuano hiyo inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Mchezo kati ya Ghana na Cape Verde ulifanyika mjini Port Elizabet

Mechi nyingine hii leo itazikutanisha wenyeji wa michuano hii, Afrika Kusini kwa kupambana na Mali mjini Durban.