Burkina Faso,Togo zapambana robo fainali

Image caption Mchezaji wa Burkina Faso

Timu za Burkina Faso na Togo zinamenyana vikali katika mchezo wa pili kukamilisha michezo ya robo fainali nchini Afrika Kusini.

Mpaka sasa Burkina Faso inaoongoza kwa goli moja lililofungwa dakika za nyongeza, kufuatia mpira wa kona.

Mchezo unaelekea ukingoni kabisa, huku ikionyesha kuwa Togo imeondolewa katika michuano hiyo.

Burkina Faso kucheza hatua hii ilifuzu kutoka kundi C, ilipoongoza, huku Togo ikiibuka kutoka kundi D ikiwa mshindi wa pili.Kundi la Burkina Faso lilikuwa na timu za Nigeria, Zambia na Ethiopia. Timu za Zambia na Ethiopia zilitolewa katika hatua ya makundi.

Kwa upande wa Togo, ilikuwa katika kundi lililokuwa na timu za Ivory Coast, Tunisia na Algeria. Timu za Tunisia na Algeria ziliyaaga mashindano hayo kwa kutolewa katika hatua ya awali ya makunZambia

Kwa upande wa Togo mchezaji wa kimataifa, Emmanuel Adebayor ndiye atakayekiongoza kikosi cha timu hiyo kupigania nafasi ya kucheza nusu fainali.