Nigeria, Ivory Coast hapatoshi leo

Image caption Yaya Toure na Drogba wachezaji wa Ivory Coast

Leo ni mchuano mkali zaidi unaotarajiwa kuonekana kati ya Ivory Coast na Nigeria, ukiwa ni mchezo wa kwanza katika kundi la pili, hatua ya robo fainali.

Ivory Coast ilifuzu kucheza hatua ya robo fainali ikitokea kundi D baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi hilo, huku Nigeria ikiibuka mshindi wa pili kutoka kundi C.

Image caption Obi Mikel mchezaji wa Nigeria

Ni mpambano ambao mashabiki wengi walitaka kuushuhudia katika hatua ya fainali. Hata hivyo timu hizo zimejikuta zikikutana katika hatua hii ya robo fainali.

Timu itakayoshinda ndiyo itasonga mbele hatua ya nusu fainali.

Baada ya mchuano huu Burkina Faso mshindi wa kwanza wa kundi C atapambana na Togo kutoka kundi D.