Burkina Faso Kijogoo, waibwaga Ghana

Image caption Wachezaji wa Burkina Faso

Burkina Faso, imetinga fainali baada ya kuilaza Ghana kwa njia ya mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika dakika 120 za mchezo, ukiwa ni mchezo wa pili wa nusu fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Ghana ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa kucheza fainali, walishindwa kutamba mbele ya vijana wa Burkina Faso na kulazimika mikwaju ya penalti inatumika.

Ghana walipata penalti mbili tu, huku mbili zikipigwa nje na moja ikipanguliwa na mlinda mlango wa Burkina Faso.

Sasa Ghana itachuana na Mali kumtafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.

Jumapili, ndiyo siku yenyewe ya kujulikana bingwa. Je, ni Nigeria au Burkina Faso? Dakika 90 zitatoa jibu la kitendawili hicho.