Ghana 1 Burkina Faso 1

Image caption Timu ya Ghana

Mchezo kati ya Ghana na Burkina Faso, bado ni sare ya 1-1, ukiwa ni mchezo wa pili wa nusu fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Goli la Ghana limefungwa na Mubarak Wakaso kwa njia ya penalti katika dakika ya 13, baada ya mshambuliaji wa Ghana Atsu kuangushwa katika eneo la hatari. Goli la Burkina Faso limefungwa na Aristides Bance katika dakika ya 60 ya mchezo.

Mpambano huu ulimalizika dakika 90 kwa sare ya bao 1-1. Hivyo kulazimika kuongezwa dakika 30.

Katika kipindi hicho cha nyongeza Burkina Faso ndiyo ilifanya mashmbulizi mengi zaidi katika lango la Ghana, ambapo goli lililokuwa limefungwa na Burkina Faso kipindi hicho cha nyongeza, lilikataliwa kwa madai ya mfungaji kumchezea vibaya mlinzi wa Ghana.

Dakika 120 zimemalizika kwa sare hiyo hiyo ya bao 1-1. Sasa ni wakati wa mikwaju ya penalti.