Messi asaini kandarasi mpya na Barcelona

Image caption Lionell Messi

Lionel Messi amesaini mkataba mpya wa miaka miwili zaidi kusalia na klabu ya Barcelona.

Kufuatia uamuzi huo, Messi sasa atasalisa na Barcelona hadi Juni mwaka wa 2018.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na mitano kutoka Argentina, amevunja rekodi kadhaa akiwa na klabu hiyo katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Mwaka uliopita Messi alifunga jumla ya magoli tisini na moja.

Messi alisaini kandarasi hiyo mapema siku ya Alhamisi baada ya Carles Puyol na Xavi, ambao tayari walikuwa wamesaini mikataba ya kuongeza kandarasi yao na Barcelona.

Wachezaji hao wawili sasa watasalia na Barcelona hadi mwaka wa 2016.