Arsenal wafunga 2-0 lakini watolewa.

Image caption Olivier Giroud afunga bao

Licha ya kuifunga Bayern Munich ya Ujerumani mabao mawili kwa bila ugenini, Arsenal waondolewa katika mashindano ya Klabu bingwa bara Ulaya.

Hii ni kwa sababu katika mechi ya awali iliyochezwa wiki mbili zilizopita katika Uwanja wa Emirates, Arsenal walifungwa magoli 3-1 na Bayern.

Mchezaji Olivier Giroud aliipatia 'The Gunners' goli lao la kwanza katika dakika ya 15 baada ya pasi safi kutoka kwa Theo Walcott.

Kufuatia bao hilo Arsenal wakawa wanahitaji magolo mengine mawili ili kumaliza mechi wakuwa juu kwa 3-0.

Mlinda lango wa Arsenal Lukasz Fabianski alifanya kazi ya ziada kwani alipangua mikwaju kadhaa kutoka kwa mshambulizi matata Arjen Robben hivyo kumnyima nafasi ya kuifungia Bayern Munich goli lolote.

Lakini baada ya mechi , Bayern Munich ndio walifaulu kuingia hatua ya robo fainali.